Brought to you by
Wadau wakutana kujadili jinsi ya kuanza uzalishaji mkubwa wa teknolojia ya kupambana na sumukuvu, Aflasafe TZ, nchini Tanzania

Warning: Undefined variable $string in /home/aflasafe/public_html/wp-content/themes/aflasafe/functions.php on line 561
Press Releases

Wadau wakutana kujadili jinsi ya kuanza uzalishaji mkubwa wa teknolojia ya kupambana na sumukuvu, Aflasafe TZ, nchini Tanzania

September 3, 2018

News item in English

DAR ES SALAAM, TANZANIA, Septemba 3, 2018 – Tanzania inajiunga na mataifa mengine barani Afrika katika kukabiliana na sumukuvu kwa kuingiza teknolojia ya kukabiliana na tatizo hilo kwenye chakula cha binadamu na mifugo.

Sumukuvu ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya kansa.

Kwa kutumia teknolojia hiyo inayotambuliwa kama Aflasafe TZ, Tanzania itajihakikishia kuwa na chakula salama kwa matumizi ya ndani na kufikia kiwango hitajika cha usafirishaji wa mazao nje ya nchi.

Teknolojia hiyo ilitengenezwa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo cha Tropiki (IITA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo nchini kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani, USAID.

Aidha mchakato wa kusajili teknolojia hiyo kwenye mamlaka ya Taasisi ya ukaguzi na udhibiti wa viwatilifu (TPRI) unakaribia kukamilika na huamishaji wa teknolojia kutoka IITA kwa ajili ya kuzalisha kwa wingi kumefanyika kupitia taasisi ya Aflatoxin Technology Transfer and Commercialisation initiative (ATTC) ili wakulima wafaidike.

ATTC imetengeneza mkakati wa kuwezesha Aflasafe kuzalishwa kibiashara kwa msaada wa kiufundi wa Shirika la Kimataifa la Dalberg Global Development Advisors and Chemonics. Mkakati huo ni pamoja na kuangalia ukubwa wa soko, utengenezaji wake na namna ya usambazaji unaotakiwa.

Pia mkakati huo umetazama kwa makini uwekezaji katika bidhaa hiyo na pia namna ya kuifikisha Aflasafe mikoani.

Katika kufanikisha hilo, IITA na washirika wake wameandaa Jukwaa la wawekezaji Jumatatu Septemba 3, 2018 ili kubadilishana taarifa za kitafiti zilizofanyika na matokeo yake na wadau wengine ili kutambulisha fursa za kibiashara katika utengenezaji, usambazaji na mauzo ya teknolojia ya Aflasafe. Mkutano huo utajumuisha watunga sera, sekta ya umma, sekta binafsi, watafiti, wakulima na washirika wa maendeleo.

“Mkutano huu ni muhimu katika juhudi za kupunguza tatizo la sumukuvu nchini Tanzania. Baada ya miaka sita ya utafiti, Aflasafe TZ ipo tayari kwa matumizi. Kwa hiyo tutatoa azimio la pamoja na kuweka mkakati wa ushirikiano utakaowezesha Aflasafe kuwafikia wakulima wote wa mahindi na karanga,” alisema Mkurugenzi Mtendaji ATTC, Abdou Konlambigue.

Sumukuvu ni sumu mbaya ambayo haina rangi, harufu, wala ladha, inajulikana kwa kuleta madhara kwa binadamu kamavile kansa ya ini. Huingia mwilini kupitia njia ya chakula, aidha ikiwa kwa wingi husababisha kifo.

Sumukuvu pia husababisha udumavu kwa watoto na hupunguza kinga za mwili. Mifugo pia huathiriwa na sumukuvu. Pia, sumukuvu uhathiri soko la ndani na nje ya nchi.

Aflasafe imetengenezwa kwa kutumia fangasi au kuvu asilia jamii ya ‘’Aspergillus fungi’’ ambaye hupatikana kwenye udongo na masalia ya karanga na mahindi shambani.

Aflasafe inamjumuiko wa fangasi wasio na uwezo wa kuzalisha sumukuvu, fangasi hawa hupingana na kuwaondoa fangasi wanaozalisha sumukuvu, hivyo husaidia kupunguza sumukuvu kwa asilimia 80 hadi 90 katika mazao ya mahindi na karanga.

“Teknolojia ya Aflasafe awali ilitengenezwa na Wizara ya Kilimo ya Marekani kupitia taasisi yake ya Huduma za Utafiti wa Kilimo (USDA‒ARS). IITA na washirika wake wamekuwa wakitafuta namna ya kuiwezesha kufanyakazi katika nchi za Afrika kwa lengo la kujihakikishia usalama wa chakula. Teknolojia hii imeshasajiliwa na ipo sokoni katika nchi ya Burkina Faso, Ghana, Nigeria, Kenya, Senegal na Gambia,” anasema Mkurugenzi wa Afrika Mashariki wa IITA, Victor Manyong.

Punde mfumo sahii wa uzalishaji ukianzishwa, Tanzania itapiga hatua kubwa katika kuhakikisha usalama wa chakula kwa wananchi na kupunguza magonjwa yanayotokana au sababishwa na sumukuvu. Pia nchi itakuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha bidhaa za ziada nje ya nchi na hivyo kutengeneza ajira na kipato kwa ajili ya wakulima na nchi kwa ujumla.

Kwataarifa zaida wasiliana na: Catherine Njuguna, IITA Eastern Africa, +255 767 361 255, e-mail: c.njuguna@cgiar.org

LINKS

Kuhusu IITA–tembele tovuti www.iita.org

The International Institute of Tropical Agriculture (IITA) is a not-for-profit institution that generates agricultural innovations to meet Africa’s most pressing challenges of hunger, malnutrition, poverty, and natural resource degradation. Working with various partners across sub-Saharan Africa, we improve livelihoods, enhance food and nutrition security, increase employment, and preserve natural resource integrity. IITA is a member of CGIAR, a global agriculture research partnership for a food secure future


PDF

2 Replies to “Wadau wakutana kujadili jinsi ya kuanza uzalishaji mkubwa wa teknolojia ya kupambana na sumukuvu, Aflasafe TZ, nchini Tanzania”

    1. Thank you for your interest in our product. We’re at the early stages of commercialising Aflasafe in Tanzania, in search of suitable partner organisations, as you will see here: https://aflasafe.com/2019/02/02/paving-the-path-to-commercialisation-aflasafe-tz01-registered-to-fight-aflatoxin-in-tanzania/

      Meantime, for Aflasafe contacts in Tanzania, please click on ‘Tanzania’ on the map here (or scroll down and click on ‘Tanzania’): https://aflasafe.com/aflasafe-where-i-am/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *